MAKALA TIME
NA CHIWAMBO
Ni siku nyingine tena
wasomaji wangu wa safu hii ya Makala Time na Chiwambo nazungumuzia “Athari za Blogu na Magazeti ya Udaku hapa
Tanzania”. Katika ulimwengu wa sasa hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi
ya vyombo vya habari kutoka mfumo wa zamani wa urushaji matangazo yaani “Analogia” na kuingia mfumo mpya wa urushaji matangazo
kwa vyombo vya habari yaani “Digital” mabadiliko hayaepukiki katika tasnia ya
vyombo vya habari nchini.
Kutokana na hilo,
Tanzania tumeshuhudia mapinduzi haya ya vyombo vya habari na kutamba kwa Blogu
na Wavuti tofauti tofauti ambazo zilizo nyingi huondeshwa bila kuzilipia.
Mapindizi haya ya vyombo vya habari yameleta mfumuko wa fikra tofauti tofauti
katika uandishi wa makala na taarifa ndani ya
blogu zetu.
Utafiti uliofanywa na Mlipa Media Group inayomiliki
Chiwambo’s Blog inaonyesha wazi kwamba zaidi ya asilimia 60% ya blogu
zinazorusha habari hapa Tanzania ni blogu za Udaku zinazojihushisha na urushaji
wa picha za ngono, Habari za mapenzi, pamoja na urushaji wa habari ambazo
hazina ukweli. Pamefikia mahari hata wasanii wanapoandaa video zao picha
hurushwa wakimaanisha kitu tofauti na uhalisia.
Malalamiko kama haya
yamethibitishwa siku ya alhamisi pale msanii wa Bongo (Jina Limehifadhiwa)
alipojitokeza mbele ya chombo cha habari cha Clouds FM kipindi kinachorushwa na
Mirrard Ayo, kupinga madai ya Blogu hizo kwamba picha hizo zimepigwa wakiwa
wanafanya mapenzi kumbe ilikuwa ni maandalizi ya video yake mpya
aliyomshirikisha mchezaji wa mpira maarufu hapa Tanzania.
Athari
za Blogu na Wavuti kwa wanajamii
Blogu kwa sasa zimekuwa
ni kama vituo vya kurushia habari za Ngono, Video za ngono, Habari za
Uchonganishi na za uzandiki. Pamefikia mahari hata zile Wavuti na Blogu zilizotegemewa
hapa Tanzania kwa kurusha habari za ukweli na uhakika nazo zimegeuka na kurusha
habari za udaku ikiwemo picha za nusu uchi au zinazoonyesha sehemu za siri za
wanawake.
Wanaoathiriwa zaidi na
picha hizi ni wanawake pamoja na wanafunzi. Pamefikia mahari mtu maarufu
asimamapo na mwanamke au mwanaume anapigwa picha na kurushwa mtandaoni. Swali
la kujiuliza, tunaelekea wapi wanahabari wenzangu? Haya ni madhara ya mtu kujua
kusoma na kuandika na kujipachika kuwa yeye ni mwandishi wa habari. Yaani mtu
akiweza kuandika barua naye hujiita ni mwanahabari.
Matokeo yake ndio haya
yanayoonekana leo. Blogu kama zingetumika ipasavyo kwa kuwahabarisha Watanzania
wenzetu habari muhimu tungeweza kuendelea. Zipo habari nyingi za kurusha hapa
Tanzania hasa huko vijijini. Magazeti, Wavuti na Blogu zetu zimeshindwa
kuwafikia Watanzania waliopo vijijini ambao hushindia mihogo na uji au mlo
mmoja kwa siku. Huduma zimekosekana, miundombinu kama barabara nazo ni aibu
upu. Maisha ya Mtanzania leo ni ajabu, wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi
yao.
Kwanini habari kama
hizi zisirushwe ili serikali ione nini inachowafanyia wananchi wao. Ijapokuwa
kuna Uhuru wa kutoa na kupokea habari, hatuna budi vyombo vyetu kuwa vyombo vya
habari vya watanzania “The voice of the voiceless”. Badala yake tumevigeuza vyombo hivi na kuwa
vituo vya kuandika habari za ngono.
Kama leo hii
ningeulizwa swali moja tu na mtu yeyote kuhusu nini kinachokukera ningesema “Vyombo
vya Habari vya Udaku hasa Blogu” na ningependekeza vifungiwe ili kulinda utu wa
watu wetu. Hivi jiulize swali moja tu. Je ungependa watoto na wajukuu wako
wazione picha zako za ngono? Huko ndiko
tunakoelekea kwa sasa.
Athari za blogu hizi ni
kwamba, tunawafundisha watoto wetu kuingia katika ngono na biashara ya ngono
wakiwa na umri mdogo sana. Hivi kama wewe ni mwandishi wa blogu, utajisikiaje
pale utapoikuta picha ya mtoto wako imetupiwa pale ndani ya blogu yako au
nyinginezo?
Wanafunzi
na picha za ngono mtandaoni
Wanafunzi wetu kuanzia
sekondari hadi vyuo vikuu imekuwa ni fasheni kwa baadhi yao kupiga picha za
uchi na ngono na kuwapa wanablogu au kuzivujisha mtandaoni. Wasomi wa leo na wa
jana ni tofauti kabisa. Wasomi wa jana waliheshimu sana utu wao na tamaduni za
kitanzania lakini wa leo hawajiheshimu baadhi yao hasa wasomi wetu wa kike.
Hivi baba yako akibahatika kuiona picha yako ukiwa uchi au unafanya ngono atajisikiaje
au wewe utajionaje? Hao ndio wasomi wetu
wa leo. Somo la maadili limekuwa kikwazo kwao. Tunatengeneza taifa la weusi
lenye giza mbele yake.
Nini kifanyike kuzuia uvunjifu wa sheria
Swala kubwa ni
wanablogu wenyewe kujiheshimu kwanza. Kuthamini watu wengine na kujithamini
wenyewe. Wanablogu wawe wakwanza katika kupinga urushaji wa picha za ngono
zinazozidi kusambaa mtandaoni siku hadi siku. Mwanablogu pekee ndiye anayeweza
kuzuia blogu yake isiweke picha za ngono ili kuweza kuzuia wimbi la watoto
wadogo kutembelea kwenye picha kama hizo.
Kitu cha ajabu ni
kwamba baadhi ya hao wanaorusha na kuongoza blogu hawajui sheria za kujilinda
pale watapokubwa na kesi juu ya wanachokiandika yaani “Law of Defamation and its element.
Haya
yote ni madhara ya mfumo wetu wa elimu na inaonyesha namna gani watanzania
hawajakombolewa na elimu. Bado tupo ugenini katika elimu. Tunafanya elimu yetu
kama kitu kisicho na umuhimu. Tunapeleka wapi elimu yetu? Tunatengeneza “Taifa
la Vilaza, Mambumbumbu, na Majuha” na hao ndio viongozi wetu hapo baadaye sisi
tutapoaga na kuondoka.
Imeandikwa na Ausi
Chiwambo
E-mail: ausichiwambor@gmail.com
Phone No. 0753110740