Saturday, November 16, 2013

BLOGU ZA TZ ZAGEUZWA VITUO VYA KURUSHA PICHA ZA UCHI NA NGONO?

MAKALA TIME NA CHIWAMBO
Ni siku nyingine tena wasomaji wangu wa safu hii ya Makala Time na Chiwambo nazungumuzia “Athari za Blogu na Magazeti ya Udaku hapa Tanzania”. Katika ulimwengu wa sasa hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya vyombo vya habari kutoka mfumo wa zamani wa urushaji matangazo yaani “Analogia”  na kuingia mfumo mpya wa urushaji matangazo kwa vyombo vya habari yaani “Digital” mabadiliko hayaepukiki katika tasnia ya vyombo vya habari nchini.

Kutokana na hilo, Tanzania tumeshuhudia mapinduzi haya ya vyombo vya habari na kutamba kwa Blogu na Wavuti tofauti tofauti ambazo zilizo nyingi huondeshwa bila kuzilipia. Mapindizi haya ya vyombo vya habari yameleta mfumuko wa fikra tofauti tofauti katika uandishi wa makala na taarifa ndani ya  blogu zetu.

Utafiti  uliofanywa na Mlipa Media Group inayomiliki Chiwambo’s Blog inaonyesha wazi kwamba zaidi ya asilimia 60% ya blogu zinazorusha habari hapa Tanzania ni blogu za Udaku zinazojihushisha na urushaji wa picha za ngono, Habari za mapenzi, pamoja na urushaji wa habari ambazo hazina ukweli. Pamefikia mahari hata wasanii wanapoandaa video zao picha hurushwa wakimaanisha kitu tofauti na uhalisia.

Malalamiko kama haya yamethibitishwa siku ya alhamisi pale msanii wa Bongo (Jina Limehifadhiwa) alipojitokeza mbele ya chombo cha habari cha Clouds FM kipindi kinachorushwa na Mirrard Ayo, kupinga madai ya Blogu hizo kwamba picha hizo zimepigwa wakiwa wanafanya mapenzi kumbe ilikuwa ni maandalizi ya video yake mpya aliyomshirikisha mchezaji wa mpira maarufu hapa Tanzania.

Athari za Blogu na Wavuti kwa wanajamii
Blogu kwa sasa zimekuwa ni kama vituo vya kurushia habari za Ngono, Video za ngono, Habari za Uchonganishi na za uzandiki. Pamefikia mahari hata zile Wavuti na Blogu zilizotegemewa hapa Tanzania kwa kurusha habari za ukweli na uhakika nazo zimegeuka na kurusha habari za udaku ikiwemo picha za nusu uchi au zinazoonyesha sehemu za siri za wanawake.

Wanaoathiriwa zaidi na picha hizi ni wanawake pamoja na wanafunzi. Pamefikia mahari mtu maarufu asimamapo na mwanamke au mwanaume anapigwa picha na kurushwa mtandaoni. Swali la kujiuliza, tunaelekea wapi wanahabari wenzangu? Haya ni madhara ya mtu kujua kusoma na kuandika na kujipachika kuwa yeye ni mwandishi wa habari. Yaani mtu akiweza kuandika barua naye hujiita ni mwanahabari.

Matokeo yake ndio haya yanayoonekana leo. Blogu kama zingetumika ipasavyo kwa kuwahabarisha Watanzania wenzetu habari muhimu tungeweza kuendelea. Zipo habari nyingi za kurusha hapa Tanzania hasa huko vijijini. Magazeti, Wavuti na Blogu zetu zimeshindwa kuwafikia Watanzania waliopo vijijini ambao hushindia mihogo na uji au mlo mmoja kwa siku. Huduma zimekosekana, miundombinu kama barabara nazo ni aibu upu. Maisha ya Mtanzania leo ni ajabu, wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao.

Kwanini habari kama hizi zisirushwe ili serikali ione nini inachowafanyia wananchi wao. Ijapokuwa kuna Uhuru wa kutoa na kupokea habari, hatuna budi vyombo vyetu kuwa vyombo vya habari vya watanzania “The voice of the voiceless”.  Badala yake tumevigeuza vyombo hivi na kuwa vituo vya kuandika habari za ngono.

Kama leo hii ningeulizwa swali moja tu na mtu yeyote kuhusu nini kinachokukera ningesema “Vyombo vya Habari vya Udaku hasa Blogu” na ningependekeza vifungiwe ili kulinda utu wa watu wetu. Hivi jiulize swali moja tu. Je ungependa watoto na wajukuu wako wazione picha zako za ngono? Huko  ndiko tunakoelekea kwa sasa.

Athari za blogu hizi ni kwamba, tunawafundisha watoto wetu  kuingia katika ngono na biashara ya ngono wakiwa na umri mdogo sana. Hivi kama wewe ni mwandishi wa blogu, utajisikiaje pale utapoikuta picha ya mtoto wako imetupiwa pale ndani ya blogu yako au nyinginezo?

Wanafunzi na picha za ngono mtandaoni
Wanafunzi wetu kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu imekuwa ni fasheni kwa baadhi yao kupiga picha za uchi na ngono na kuwapa wanablogu au kuzivujisha mtandaoni. Wasomi wa leo na wa jana ni tofauti kabisa. Wasomi wa jana waliheshimu sana utu wao na tamaduni za kitanzania lakini wa leo hawajiheshimu baadhi yao hasa wasomi wetu wa kike. Hivi baba yako akibahatika kuiona picha yako ukiwa uchi au unafanya ngono atajisikiaje au wewe utajionaje?  Hao ndio wasomi wetu wa leo. Somo la maadili limekuwa kikwazo kwao. Tunatengeneza taifa la weusi lenye giza mbele yake.

Nini  kifanyike kuzuia uvunjifu wa sheria
Swala kubwa ni wanablogu wenyewe kujiheshimu kwanza. Kuthamini watu wengine na kujithamini wenyewe. Wanablogu wawe wakwanza katika kupinga urushaji wa picha za ngono zinazozidi kusambaa mtandaoni siku hadi siku. Mwanablogu pekee ndiye anayeweza kuzuia blogu yake isiweke picha za ngono ili kuweza kuzuia wimbi la watoto wadogo kutembelea kwenye picha kama hizo.

Kitu cha ajabu ni kwamba baadhi ya hao wanaorusha na kuongoza blogu hawajui sheria za kujilinda pale watapokubwa na kesi juu ya wanachokiandika yaani “Law of Defamation and its element.

Haya yote ni madhara ya mfumo wetu wa elimu na inaonyesha namna gani watanzania hawajakombolewa na elimu. Bado tupo ugenini katika elimu. Tunafanya elimu yetu kama kitu kisicho na umuhimu. Tunapeleka wapi elimu yetu? Tunatengeneza “Taifa la Vilaza, Mambumbumbu, na Majuha” na hao ndio viongozi wetu hapo baadaye sisi tutapoaga na kuondoka.
Imeandikwa na Ausi Chiwambo

Phone No. 0753110740

Monday, December 31, 2012

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI
Kila siku tunaimba mungu ibaliki Tanzania, watanzania wanaitikia“ ameeeeeeeeeeeeee”. Hii ndiyo Tanzania yetu. Mahakama inaonekana inapoteza kodi nyingi ksimamia kesi zisizo na kichwa wala miguu. Nasikitika kuona katiba ya Tanzania ya muungano ya 1977 Ibara ya 46-(1) inasema “Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshtaki au kuendesha mashtaka ya aina yeyote juu  yake mahakamani kwa ajili ya kosa la jinai”.
(2) “Wakati wote Rais atakapokuwepo madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhsiwa kufunga mahakama shauri kuhsu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama Raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku therathini kabla ya shauri kufungliwa mahakamani., Rais atapewa au atakuwa ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kfuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anuani yake ya mahari anopoishihuyo mdai na jambo hasa analodai”.
Katika ibara hii ya pili inampa Rais kinga kubwa dhidi ya madaraka ya Raisi. Kwa Tanzania inaonekana ukiwa Rais wan chi hii hwezi kushtakiwa na mahakama yeyote hata kama ukiboronga katika uongozi wako. Ukiamua kuua ni ruksa, kuwa mwizi ni ruksa, kufanya uhaini ni ruksa, uza madawa ya kulevya Ruksa, agiza watu Fulani wawekwe ndani Ruksa, kumpa kinga ya mtu kushtakiwa Ruksa? Jamani kweli tutafika kwa msingi huu. Kwa hali hii kwanini tusiseme kuwa Rais anaonekana kama yupo juu ya sheria na ndio ukweli halisi?
Kwa msingi huu watanzania kupata haki ya kumshtaki Rais itakuwa ndoto hadi tu pale katiba hii mpya inayotarajiwa kuandikwa 2014 na kupitishwa na wananchi itakapokamilika. Kwa sasa Rais katika awamu yake ya pili ya uchaguzi (Ungwe ya pili), wakati wa kampeni zake hata akitoa kauli za vitisho, Rushwa Takatifu, Kuiba kura na madudu mengine hawezi kushtakiwa hata kidogo? Jibu lipo katika ibara ya 46-(1 & 3).
(3), “isipokuwa kama akiacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A.-(1) itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa ameshika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba hii”.
Hapa ndipo ninaposema kuwa ukiwa Rais fanya chochote hata ukiondoka nani atakushtaki wakati una kinga “madhubuti” kutoka kwenye katiba yetu inayotuongoza ya mwaka 1977. kwa msingi huu hata mimi ijapokuwa sikuwa na ndoto ya kuingia kwenye siasa, unaweza kukuta nashawishika kuomba au Kutangaza nia miaka ya Mbele ili na mimi niwe Rais. Kwani nikiwa Rais nani atanishtaki? Kama wabunge kumi nawapendekeza mimi au kuwateua, chama changu kitakuwa na wabnge wengi wa kunitetea na hata nikifanya madudu nani ataniondoa?
Hata majaji wa mahakama kuu wenyewe nawateua mimi, mwanasheria mkuu namteua mimi na kumpa baraka yangu, Mkuu wa TAKUKURU namteua mimi, Kamishana wa Haki za binadamu na uongozi bora ni mimi. Hata wale wanaovaa zile nguo za kutisha wakuu wao nawateua mimi na kuwapendekeza vyeo mimi, mawaziri mimi, hata wale sisimizi nawateua mimi, hivi unadhani kuna mtu anaweza kunifungulia mashtaka wakati mimi nina kinga mzito kutoka kwenye katiba na wale niliowateua?
Hata kamishna wa haki za binadamu akipata taarifa zangu mbaya nilizofanya ataniambia Bwana Mkubwa hapa umebolonga mzazi. Lakini mimi ndio mwamuzi wa kusema nipelekwe mahakamani au nisipelekwe. Na kama waking’ang’ania watakuwa wanajihangaisha tu kwani hata leo hii nikimaliza uongozi wang nitaendelea kula bata (Msemo wa vijiweni yaani kula raha).
Na hata waqkipenda kunipeleka mahakamani Ibara ya 45 (1-a) Rais mpya hana haki ya kutoa msamaha juu ya shauri lolote lililopo mahakamani. Hivi kwa msingi huu kwanini nisitangaze nia na mimi. Lakini mimi si mwanasiasa na sina chama hata kimoja.
Hata ukiangalia namna ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais nayo ni utata mtupu. Kwa hiyo hapa simahanishi ukiwa Rais wan chi hii ufanye mambo kinyume na katiba, kwani ukitenda hayo kama Rais Bunge litakushtaki kama inavyoonyesha Ibara ya 46 (A). na ujue kwamba hata Waanchi wakichoka wanaweza kuandamana hata ikiwa kuna sheria ya kupinga maandano, watu waneweza kuandamana ili kuondokana na uozo wa uongozi.
Ni matumaini yangu kwamba mt yeyote atayechagliwa kuwa Rais, lazima aitetee na kuilinda katiba ya Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hata kama tunaitafuta nyingine ambao mimi napendekeza vifung nilivyoviandika kwenye nakala hii viondolewe ili kupunguza kinga ya Rais ya kutoshtakiwa.
“Watanzania wa leo sio wa jana. Na watanzania wa leo sio wa kesho”. Ninamaanisha kwa sasa upeo wa watu wa kufikiri ni mkubwa kuliko zamani. Hii ni kutokana na watu wa sasa wanasoma sana nakala mbalimbali kuliko zamani. Hivi itakuwa zaidi hapo baadaye kwani shule zetu za kata zitazalisha watoto wengi wenye uelewa mkubwa kuliko leo.
Sasa naamia upande wa Ubunge. Nakumbuka miezi kadfhaa iliyopita siku ya Wanasheria Tanzania duniani na Tanzania Rais wetu Dr. J. M. Kikwete alikili na kusisitiza kuwa baadhi ya taasisi muhimu zimokosa fedha kutokana na serikali kuishiwa fedha za kuendeshea taasisi hizo ili zitoe huduma vizuri kwa wananchi.
Moja ya Taasisi iliyoathirika sana kutokana na kauli yake ni hii ya mahakama. Lakini cha kushangaza ni kwamba fedha za kusimamia Ukiukwaji wa kampen za Ubunge fedha hizo zipo. Hakuna ida kabisa. Ni sanii mtupu. Hivi leo hii serikali inaweza kutoa fedha za kusimamia kesi ya uchaguzi nchi nzima, hii ni halali na fedha hizo ni kodi za wananchi.
Wananchi wanalipa kodi, wanapeleka idara ya Mahakama ili wawapaishe majina baadhi ya watu. Tusizungumze bila mifano angalia mfano huu “Mh. Tundu Lisu alipingwa ubunge mahakamani lakini alishinda, Mnyika Dar es Salaam pia Jana tarehe 24-05-2012 alishinda kama kawaida, na baadhi ya kesi nyingi zikiwemo zile za Mwanza na maeneo mengine.
Serikali kupitia mahakama wanamaliza fedha za bure. Napendekeza itungwe sheria kali itayowabana hawa wanaoshindwa kulipia fedia zote zilizotumika na mahakama katika kuendesha kesi ya aina hiyo. Kwa mtu anayeshindwa ndiye anayepaswa kulipa. Kwa kufanya hivi fedha za wanyonge na walipa kodi zitatumika kutoa hduma nyingine badala ya kendesha fedha za wachache wanaotaka kukuza majina kisiasa.
Kwa kawaida kesi moja ya ya kupinga matokeo inayopelekwa mahakama kuu ya Tanzania husimamiwa na majaji watatu waliobobea. Wanapokuwa huko hupewa posho mbalimbali ikiwemo maradhi, chakula na mengine. Hizi ni gharamu zisizotarajiwa. Hakuna ulazima wa kuzitumia hizi. Huu mimi naona ni ubadhilifu wa fedha za Umma.
   Napendekeza kwamba mahakama zisimamie kesi nyinginezo tofauti na hizi za sasa. Kwni kuna kesi nyingi zinasubiri majaji hawa watoe hukumu yake.
NAKALA HII IMEANDIKWA NA MSOMAJI WA GAZETI LA MWANAHALISI, CHIWAMBO AUSI R, TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU). ANASOMA BA-SOCIOLOGY AND SOCIAL WORK. 0753110740 NA E-MAIL ausichiwambor@hotmail.com

BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR

BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR


BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR
Chiwambo Asi R.
Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia machafuko makubwa sana. Ikihusisha vitendo vya uchomaji wa makanisa, uhalibifu wa mali za umma, na wengine kuwekwa ndani. Hili si jambo tu la kukurupuka na kuanza kubeza sana upande mmoja kwani kila jambo ni matokeo ya mfumo Fulani.
Taasisi iliyoingia kashfa hiyo ni Taasisi ya UAMSHO ikiwa chini ya baadhi ya waislamu Zanzibar. Zanzibar wanataka nchi yao iwe huru, wakati watanganyika tunataka Zanzibar iendelee kuwa hru. Na cha kusikitisha zaidi lile baraza la usuruhisho masuala ya muungano ni raia wa Zanzibar. Hakuna Mtanganyika pale.
Ofisi inayohusika na masuala ya muungano ni ofisi ya Makamu wa rais. Na hata walio kwenye kamati hiyo wote ni  Wazanzibar. Hivi unadhani kama ikitokea wao hawautaki muungano unadhani kwamba wataleta majibu yaliyo sahihi? Hawa ni viongozi wetu, tuendelee kuwaamini kwani tushike ule usemi usemao kiongozi ni kioo cha jamii.
Makundi yeyote yanavyoanzishwa huanza na  Hatua (stage) zake. Kila hatua inajitegemea kama ifuatavyo:-
  1. Hatua ya kwanza ya kuunda Kikundi. (Preliminary or incipiency stage). Hapa ndipo vichwa vya watu vinapogongana kimawazo juu ya kit Fulani kwenda tofauti. Viongozi hutokea ambao si rasimi na kuanza kuonesha hisia zao.
  2. hatua ya pili ambayo inahsisha kuanza kutengeneza kundi na kuongeza uelewa kwa watu (Coalescence stage). Hapa panahitaji viongozi ambao wataongeza ukaribu na watu wengine. Kipindi kingine wanazungumzia mawazo yao yote hata kupitia vyombo vya habari.
  3. hatua ya nne ambapo kikundi kimekomaa na kufikia kilele cha kundi (Institutionalization or Bureaucratization stage). Hapa viongozi wanakuwa ni wakuchaguliwa na ufata mfumo wa taasisi Fulani (chain of command). Na viongozi hao hulipwa kiasi cha fedha.
  4. Anguko. (Decline stage).hapa ni sehemu ya mwisho kabisa ambapo ni anguko ku la kundi lililoundwa katika hatua ya kwanza. Hapa kundi hili usambaratika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanikiwa kwa lengo lao, au kusambaratishwa.
Hizo ndizo hatua za makundi yanavyotokea. Hivi viongozi wetu hawakuziona hatua kama hizi? Kama kweli tunautaka muungano kwanini serikali iliwaachia uhamsho kuendesha mijadala yake huku wakijua kuwa wanazidi kulikuza zaidi kundi hili? Huu ni uasi au ni nini? Kwa upande wangu naona kwamba ni uzembe wa watu wachache ndio uliopelekea visiwa vya Zanzibar kuingia kwenye machafuko.
Kwa kiongozi yeyote aliyesomea masuala ya uongozi au jamiii lazima amezisoma hatua kama hizi na namna ya kuyasambaratisha haya makundi. Kwanini zisitumike ikiwemo njia za amani. Makundi haya yalipata uchungu zaidi pale viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali walipokamatwa na jeshi la polisi katika eneo la bunge kwa madai kuwa ni kinyume na sheria za nchi kwa kifupi nilivyoelewa mimi ni kwamba walikuwa waasi. Ni kweli kabisa.
Lakini ilipaswa itumike busara kutatua mgogoro huu badala ya vitisho. Hawa Wazanzibar walianza kudai Zanzibar ijitenge kwa muda wa miaka mingi sana. Kwa wale wenye kumbukumbu munaweza kumkumbuka yle aliyekuwa rais wa Zanzibar Ndugu Aboud Jumbe Mwinyi alivyotangaza nia ya kutaka kuvunja muungano akiwa Dodoma kwenye vikao Fulani. Kilichompata ni kuondolewa klatika nafasi hiyo.
Nyadhifa zake zote za kichama na serikali alivuliwa kufumba na kufumbua macho. Hii ni kweli kuwa uasi ulianzia muda mrefu sana. Hapo ndipo Mwalimu Nyerere aliposema kuwa tusikubali kuvunja muungano. Hata Nyerere wetu kumbe aliyajua haya mapema hasa pale kundi la G51 lilivyoanza kukua nchini Tanzania.
Kwa hiyo suala la hawa jamaa wa UAMSHO chanzo chake kimetoka mbali. Kwa hiyo kwa wakati huu ambao nchi mbalimbali zinaonyesha namna waasi wanavyoongezeka siku hadi siku, hasa nchi zile za kiarabu na baadhi ya nchi za Kiafrika, napendekeza serikali bora itumie busara zaidi katika kutatua tatizo hili badala ya vitisho na nguvu nyingi. Kweli hawa watu wapo kinyume cha sheria za nchi.
Lakini busara muhimu zaidi kuliko nguvu zaidi. Kwanini serikali isikae nao pamoja na kanza kusikiliza madai yao? Kama yana msingi kwa hatima ya nchi yetu yafanyiwe kazi. Mbona madaktari ilitumika njia kama hii. Kwanini isitumike kule Zanzibar. Inasikitisha kuona kila kukicha vituko Zanzibar mara tunataka nchi yetu.
Haya yamefugwa sana na sisi wenyewe kwani viguvugu lilipoanza hasa katika ule muswada wa maoni ya katiba mpya hawa walichana hadharani na kupinga kujadiliwa. Wakati ule likuwa muhimu kuweza kutafta njia mbadala za kutatua ili kuonyesha namna tunavyoujali muungano wetu.
Nalipenda sana Tanzania hasa hili jina zuri la Tanzania. Kwa hiyo nadhani viongozi wa serikali mutatumia wawazo haya ili kuhakikisha tunabaki na Tanzania moja, Imara na yenye amani na utulivu kama aliotuachia mwalimu Nyerere.
Powered by Chiwambo Ausi R.       

MWANAHARAKATI NA TANZANIA YA LEO

MWANAHARAKATI NA TANZANIA YA LEO


MWANAHARAKATI NA TANZANIA YA LEO
Hapo mwanzo katika kijiji kimoja kulikuwa na vijana wenye nguvu na waliopigania nchi yao kuwa huru. Nchi hiyo ilijulikana kwa jina la Kuabudika, na ilikuwa na miji mikubwa kama sita. hali ya jiji la kwanza ilikuwa sawa na yale mengine. kila kukicha nchi hii maarufu kwa utajili wa kila aina ilibadilika. maisha yalikuwa bora ya jana kuliko leo kikicha. nimesahau kuanza na neno hili "hadithi hadithi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!" hadithi hadithi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!".
yale majoho waliyozoea kuvaa kila siku wale wenye nazo ilifikia mahali bei ilipanda kiasi kwamba kama ni mfanyabiashara ndogondogo ununuapo joo moja fedha za mtajiulikuwa kwaheli. watu walilalamikia juu ya nchi yao. Nchi hii ilikuwa na sifa kubwa yenye viongozi wanaotabili nini hapo baadaye kitatokea na nani aondolewe wapi hapelekwe wapi. kiongozi aliyeamishwa akikataa kufanya hivyo hatima yake ilikuwa ni kifo tu.
Hali ilikuwa vile hadi walipozaliwa watoto mapacha watatu waliofanana kwa kila sifa. walikuwa wakakamavu, wazuri, wenye nia ya kukomboa nchi yao na walitembea wakati wote pamoja. walitumia muda wao wote kusoma kuanzia darasa la kwanza hadi la nane wakiwa na wazazi wao wateule. watoto hawa walipendana sana, walivaa sare vizuri ijapokuwa uwezo wao ulikuwa mmmmmmmmmmm.
Mungu aliwabaliki wale watoto watatu na kufahuru darasa la nane shule ya msingi Majaribu iliyoko wilaya ya Chinyauleje kata ya Kweko. walichaguliwa kuingia kidato cha kwanza na kumaliza kidato cha nne shule ya sekondari Achimwene. mungu aliwabaliki kusomea masomo ya uasikari katika kikosi maalumu. majina ya wale wote yalikuwa "HUZUNI, AMANI NA UTULIVU". baadaye walifanikiwa kwenda kikosi kingine cha masomo ya juu ya uasikari na kuwa makomando wa jeshi.
Hawakulidhika na mishahara waliyopewa kwani walikuwa na ndoto ya kuikomboa nchi yako. Vijana hawa waliamua kuacha kazi na kuendelea na masomo ya chuo kikuu. walisoma chuo kikuu cha Mwanaharakati kilichopo nchi nyingine ya Ahadi. walisoma masomo ya "BA-political science and International Relatioship".
baada ya kutunukiwa Shahada zao walirudi Nyumbani Nchi ya "Kuabudika". siku ile ilikuwa siku ya ajabu kubwa sana. vijana walifuatwa na ndege ya Wanamapinduzi. safari ilianza saa sita mchana. safari ile ilikuwa ni ya siku mbili. waliingia nchini mwao mnamo saa 8.00 mchana. nchi ilianza kutikisika ghafla kabla ndege kutua uwanja maarufu wa St. Ambuje. Mchana kukawa giza nene kama manane ya usiku. nchi ilikuwa nyeusi ikiashiria kuingia kwa wakombozi watatu kutoka Mwanaharakati university.
Ndege ilitua chini, ghafla mchana ulilejea. Kiongozi wa nchi lle maarufu kwa jina la NJETE JA KWEKULA", ALIAGIZA VIJANA WALE WATATU WAUWAWE HARAKA IWEZEKANAVYO KWANI MTABRI WAKE MAARUFU ALITABIRI KUWA VIJANA WALE WA WATATU MMOJA KATI YAO ATAKUWA MTAWALA WA NCHI LE.
ikumbukwe kuwa yule raisi alijiweka madarakani ni kiongozi wa maisha. hakukuwa na uchaguzi wa rais katika nchi ile, yeye aliteua wabunge na viongozi wote wa serikali. yeye ndiye Hakimu na jaji mkuu wa nchi ile. na wazizi wa wae watoto waliuawa na rais wakati watoto hawa wakiwa wachanga sana baada ya rais wa nchi hiyo kuwatuhumu kwa kutaka kufanya mapinduzi.
Wakiwa uwanja wa ndege wale vijana watatu waliwekwa chini ya ulinzi na kikosi maalumu cha makomandoo. ilikuwa patashika vijana wale kukamatwa. vurugu kali ilitokea. na wakati huo huo watu walikuwa wamejaa barabara zote kuzunguka kiwanja maarufu cha ndege. barabara zote zilijaa watu kwa kuwa waliona wanamapinduzi walikuwa wanaingia siku ile. vijana wale walitakiwa kuzungumza na wananchi ili kuzungumzia nini hatima ya nchi yao ambayo uchumi ulishuka kiasi kwamba thamani ya fedha ilishuka hata mkate ulikuwa haushikiki kwa bei mbaya.
wote watatu walikamatwa palepale uwanja wa ndege na kupandishwa ndege maalumu ya jeshi na ndege kupaa tena kuelekea uwanja wa dhambi tayari kwa kunyongwa kama hukumu inavyonesha.
wakati ule vyombo vya habari vilikata matangazo ghafla. wananchi walishangaa sana kuona mgeni wao anapandishwa ndege ya kijheshi na kupaa juu. ghafla mabomu ya machozi yalianza kuvuma huku na kule. watu waliuwa sana. yale yalikuwa mauaji makubwa kuliko yote Tangu nchi ile Iumbwe na Mwenyezi Mungu.
watu waliuwawa makanisani, misikitini, mitaani na maeneo yenye mkusanyiko. hali ilikuwa mbaya tena mbaya sana. watu milioni moja waliuwawa. hapo ndipo sheria mbaya zaidi zilivyoongezeka. katiba ya nchi ilibadilishwa na kunyima uhuru wa vyombo vya habari, maandamano pamoja na mikusanyiko.
siku ile ya mauaji umji ulijaa maiti kiasi kwamba watu walisema leo ndio mwisho wa dunia. Miezi ishirini na nne ilipita, hatima ya nchi haijulikani. wannchi hawajui wale wakombozi wao wamepelekwa wapi. na mtu hana haki ya kuongea juu ya mstakabali wa nchi yao. watu waliamini mungu ndiye aliyesababisha hali hiyo ya nchi. nchi ilikuwa maskini ya mwisho katika dunia ile. watu waliishi bora jana kuliko leo na walikuwa wanasubiri kufa tu maana hakukuwa na namna ya kuwezakuendesha nchi yao.
vijana wale baada ya ya safari ya siku mbili wafikishwa msitu mnene wa "CHIKANJE". msitu ule watu huwa ni chakula cha wanyama. wale askari waliopewa kazi ya kuwanyonga wale vijana watatu, walianza kuwaambia kuwa "nyinyi mlikuwa ni makomandoo wa jeshi, mliacha kazi ya uasikali kwenda masomoni ili kuikomboa nchi yetu. na rais wa nchi hii ametoa amri ya kuuawa kwenu. mnatakiwa muuawe mara moja................................................................................................................. ni amri.
mungu si athumani. mungu amtupi mja wake. wale asikari wanyongaji walikaa kikao cha ghafla. loo!!!!!!!!!!!!. askari mmoja alisema "haiwezekani watu hawa wauawe". mmmmmmmmmm! la hasha!!!!! penye nia pana njia. askari walitafakari na kufikia hatima ya wale vijana watatu. askari wale waliamua kuwaachia huru wale vijana watatu kwa masharti maalumu.
Walikaa kikao cha ghafla na wale watuumiwa watatu. waliwafungua pingu na kuanza kupanga mikakati ya kuipindua nchi. waliweka kila njia na mipangoyote ilikaa vizuri. walipanga wale watakuwa na ulinzi wa jeshi la nchi hiyo. katika mikakati yao ilikuwa ni kumteka kiongozi wa jeshi wa nchi ile na kisha kumalizia kwa rahisi. haraka haraka haina baraka, mmoja wa askari kwa cheo cha Copro Antinion Mwangatu-mbujiko. kazi ilianza mara moja.
kama mungu alipanga hivi. wananchi wa nchi ile waliamka asubuhi bila ya kuamshwa na kuanza kuandamana bila ya kiongozi. kila kijiji, katani, wilaya ,miji na majiji yaliandamana. watu walikuwa wachungu kama pilipili kichaa. Habari ndiyo hiyo kila kona ya jiji. Wananchi walibeba mabango yaliyoandikwa "MAPINDUZI NI LAZIMA, RAIS HATUKUTAKI, LAZIMA UONDOKE, PIGA UA GALAGAZA NCHI HII SI YAKO, RAIS ONDOKA TUPATE AJIRA NA  mengine mengi". kumbe hali ile ilitengenezwa na jeshi la nchi ile na wale vijana watatu wa chuo kikuu.
Askari wote wa nchi waliwatetea wananchi, hakuna aliyeuawa na askari kama ilivyokuwa mwanzo, katiba haikufuatwa kwa askari kuruhusu wananchi waandamane, na kuwapa mabango. kipindi wananchi wakiandamana jeshi la nchi hiyo ilimteka kamanda wa jeshi la nchi hiyo Meja General MWE ULI.
Rais alishangaa ghafla kuona wananchi wanakaribia kasili wakiwa na mabango ya ya maandamano pamoja na silaha kali wakisindikizwa na jeshi la nchi hiyo huku ndege za jeshi za kiita zisizo na rubani na zenye rubani zikiwa na siraha nzito nzito ikiwemo mabomu mazito mazito.
wananchi wa nchi ile walifanikiwa kuiteka ikuru na kumchoma moto Rais wa nchi ile. habari yake iliishia pale. mara ya mwisho yule rais kabla ya kifo chake alisema "KWELI NGUVU YA UMMA..................................................................................................................................................................."
LEO HII NAUKUMIWA BILA KUTAKA KISA UONGOZI WANGU ULIKUWA MBAYA" MUNGU NISAIDIE NIFIKA PAHALA PEMA PEPONI" Wananchi walisema "ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee" wengine walisema Amina". 
POWERED BY CHIWAMBO AUSI R, TEKU UNIVERSITY, 2012

MAANDAMANO YA MTWARA JANA KUHUSU KUPINGA KUSAFIRISHWA GASI YA MTWARA KENDA DAR ES SALAAM INATOA FUNDISHO GANI?

MAANDAMANO YA MTWARA JANA KUHUSU KUPINGA KUSAFIRISHWA GASI YA MTWARA KENDA DAR ES SALAAM INATOA FUNDISHO GANI?


MAANDAMANO YA MTWARA JANA KUHUSU KUPINGA KUSAFIRISHWA GASI YA MTWARA KENDA DAR ES SALAAM INATOA FUNDISHO GANI?
MAKALA TIME NA CHIWAMBO
Jana nchi nzima imepata habari juu ya maandamano yaliyotokea Mkoani  Mtwara kuhusu kupinga kusafirishwa kwa gesi yao kupelekwa jijini Dar es salaam. Kwa wale waliokosa kuangalia televisheni, Radio au kupata taarifa kwenye tovuti mbalimbali basi leo asubuhi walipata kusikia juu ya maandamano hayo kupitia magazeti ya leo asubuhi.
Swali la kujiuliza ni kwamba kwanini maandamano yametokea? Kwa nini hii ni mara ya pili kwa mtwara kuandamana ndani ya mwaka mmoja? Tatizo kubwa ni nini? Je wametimiziwa mahitaji yao kwanza kabla gesi yao haijaanzwa kuchimbwa? Kwa maana hiyo watu wengi wanaofuatilia masuala ya kitaifa na mustakabali wa Taifa letu basi atakuwa amejiuliza maswali mengi sana pengine ni tofauti na maswali yangu.
Baadhi ya Mabango yalisema “Ukiiuuaa! Tunakupeleka The Heg Gesi Haitoki, Mshua hii Gesi ni ya wamakonde tafuta ya Wakwere, Mh. Kikwete Tatizo sio Gesi Mikataba yako Noma, Gesi Kwanza Uhai Baadae, Bandari Bagamoyo Gesi Bagamoyo Viwanda Bagamoyo Mtwara wapuuz,  na linguine lilisema Gesi Ibaki au Tugawane Nchi”. Hayo ni baadhi tu ya Mabango jinsi yanavyoonyesha.
Hapa kwa sisi tuliosomea au tunaosomea masomo ya Jamii tunabaini kwamba hapo pana tatizo. Wananchi inawezekana hawajatimiziwa mahitaji yao. Kutokana na hali hiyo iliwafanya wao waandamane. Hii ni hatari kwa nchi yetu. Tukiangalia kwa undani zaidi kuhusu suala la kuwapunguzia gharama za umeme kwa wakazi wa Mtwara hiyo bado sio suruhu la matatizo ya wananchi.
Kwa kiasi kikubwa maeneo ya kusini ukianzia mkoa wa Lindi, Mtwara, na Kumalizia Ruvuma hali ya wananchi ya maendeleo ni Mbaya sana ten asana. Watu walio wengi wanaonyesha wamekata tama na mfumo wa maisha wanayoishi. Mwezi  Julai Mwaka huu nilikuwa wilaya ya Newala katika sehemu za tafiti zangu za kuizunguka Nchi yetu hasa maeneo ya vijijini.
Nyumba za wananchi wengi huko ni za Nyasi hasa vijijini. Je kuwaambia hawa watu kuwa watapunguziwa gharama za umeme wakati wanaishi nyumba za nyasi inakuja akilini kweli? Kwanini hali hii unadhani kwa nini wananchi hao  waliandamana. Zao kuu walilokuwa wanategemea kulima na kuuza ili waendeshee maisha yao ni Korosho. Hili ni zao ambalo uuzaji wake sasa unaleta wasiwasi kwa wananchi na walio wengi sasa wamekata tama kulimia hasa wale wakulima wadogo wadogo.
Kama serikali ingeboresha zao la korosho hawa wananchi wangeweza kununua bati na vifaa vingine vya ujenzi ili wapate kunufahika na punguzo la Gharama  za umeme kwa wanamtwara. Hivi mwananchi atawezaje kuweka umeme kwenye nyumba ya nyasi? Wakati huu sasa sio wa kuwadanganya wananchi. Mufanye tafiti kule vijijini kusini mwa Tanzania mutaona hali ilivyo ya kimaisha. Watu walio wengi wanaishi majumba ya majani au Nyasi kipindi kingine wengine hujenga nyumba zinazoitwa suti yaani Nyasi chini hadi juu. Eti tumwekee umeme mtu huyu inakuja akilini?
Tuangalie namna ya kutatua matatizo ya wananchi. Je wananchi wamepewa nafasi ya kusikilizwa? Je wao mapendekezo yao yanesemaje? Je timu ya washauri ilikwenda huko? Mambo mengine hayana haja ya Rais wan chi aingilie kati. Viongozi wa chini wamewajibika vipi kuwalainisha wananchi ili waweze kuruhusu gesi yao ipelekwe Dar es salaam.
Ni Matumaini yangu kuwa utaweza kukaa na kutafakari zaidi wewe Mtanzania kwamba kifanyike nini ili kuzuia maandamano ya wananchi kila kukicha. Kuna mtu alikuwa anatania eti kwa sasa pamefikia mahari hata watoto nao wanaweza kuandamana kumshinikiza baba awe anarudi nyumbani mapema. Why?
Maoni yako Tima Kwa barua pepe au hapo chini ausichiwambor@hotmail.com