MAANDAMANO YA MTWARA JANA KUHUSU KUPINGA KUSAFIRISHWA GASI YA MTWARA KENDA DAR ES SALAAM INATOA FUNDISHO GANI?
MAANDAMANO
YA MTWARA JANA KUHUSU KUPINGA KUSAFIRISHWA GASI YA MTWARA KENDA DAR ES SALAAM
INATOA FUNDISHO GANI?
MAKALA
TIME NA CHIWAMBO
Jana
nchi nzima imepata habari juu ya maandamano yaliyotokea Mkoani Mtwara kuhusu kupinga kusafirishwa kwa gesi
yao kupelekwa jijini Dar es salaam. Kwa wale waliokosa kuangalia televisheni,
Radio au kupata taarifa kwenye tovuti mbalimbali basi leo asubuhi walipata
kusikia juu ya maandamano hayo kupitia magazeti ya leo asubuhi.
Swali
la kujiuliza ni kwamba kwanini maandamano yametokea? Kwa nini hii ni mara ya
pili kwa mtwara kuandamana ndani ya mwaka mmoja? Tatizo kubwa ni nini? Je wametimiziwa
mahitaji yao kwanza kabla gesi yao haijaanzwa kuchimbwa? Kwa maana hiyo watu
wengi wanaofuatilia masuala ya kitaifa na mustakabali wa Taifa letu basi
atakuwa amejiuliza maswali mengi sana pengine ni tofauti na maswali yangu.
Baadhi
ya Mabango yalisema “Ukiiuuaa! Tunakupeleka The Heg Gesi Haitoki, Mshua hii
Gesi ni ya wamakonde tafuta ya Wakwere, Mh. Kikwete Tatizo sio Gesi Mikataba yako
Noma, Gesi Kwanza Uhai Baadae, Bandari Bagamoyo Gesi Bagamoyo Viwanda Bagamoyo
Mtwara wapuuz, na linguine lilisema Gesi
Ibaki au Tugawane Nchi”. Hayo ni baadhi tu ya Mabango jinsi yanavyoonyesha.
Hapa
kwa sisi tuliosomea au tunaosomea masomo ya Jamii tunabaini kwamba hapo pana
tatizo. Wananchi inawezekana hawajatimiziwa mahitaji yao. Kutokana na hali hiyo
iliwafanya wao waandamane. Hii ni hatari kwa nchi yetu. Tukiangalia kwa undani
zaidi kuhusu suala la kuwapunguzia gharama za umeme kwa wakazi wa Mtwara hiyo
bado sio suruhu la matatizo ya wananchi.
Kwa
kiasi kikubwa maeneo ya kusini ukianzia mkoa wa Lindi, Mtwara, na Kumalizia Ruvuma
hali ya wananchi ya maendeleo ni Mbaya sana ten asana. Watu walio wengi
wanaonyesha wamekata tama na mfumo wa maisha wanayoishi. Mwezi Julai Mwaka huu nilikuwa wilaya ya Newala
katika sehemu za tafiti zangu za kuizunguka Nchi yetu hasa maeneo ya vijijini.
Nyumba
za wananchi wengi huko ni za Nyasi hasa vijijini. Je kuwaambia hawa watu kuwa
watapunguziwa gharama za umeme wakati wanaishi nyumba za nyasi inakuja akilini
kweli? Kwanini hali hii unadhani kwa nini wananchi hao waliandamana. Zao kuu walilokuwa wanategemea
kulima na kuuza ili waendeshee maisha yao ni Korosho. Hili ni zao ambalo uuzaji
wake sasa unaleta wasiwasi kwa wananchi na walio wengi sasa wamekata tama kulimia
hasa wale wakulima wadogo wadogo.
Kama
serikali ingeboresha zao la korosho hawa wananchi wangeweza kununua bati na
vifaa vingine vya ujenzi ili wapate kunufahika na punguzo la Gharama za umeme kwa wanamtwara. Hivi mwananchi
atawezaje kuweka umeme kwenye nyumba ya nyasi? Wakati huu sasa sio wa
kuwadanganya wananchi. Mufanye tafiti kule vijijini kusini mwa Tanzania mutaona
hali ilivyo ya kimaisha. Watu walio wengi wanaishi majumba ya majani au Nyasi
kipindi kingine wengine hujenga nyumba zinazoitwa suti yaani Nyasi chini hadi
juu. Eti tumwekee umeme mtu huyu inakuja akilini?
Tuangalie
namna ya kutatua matatizo ya wananchi. Je wananchi wamepewa nafasi ya
kusikilizwa? Je wao mapendekezo yao yanesemaje? Je timu ya washauri ilikwenda
huko? Mambo mengine hayana haja ya Rais wan chi aingilie kati. Viongozi wa
chini wamewajibika vipi kuwalainisha wananchi ili waweze kuruhusu gesi yao ipelekwe
Dar es salaam.
Ni
Matumaini yangu kuwa utaweza kukaa na kutafakari zaidi wewe Mtanzania kwamba
kifanyike nini ili kuzuia maandamano ya wananchi kila kukicha. Kuna mtu alikuwa
anatania eti kwa sasa pamefikia mahari hata watoto nao wanaweza kuandamana
kumshinikiza baba awe anarudi nyumbani mapema. Why?
Maoni yako Tima Kwa barua pepe au hapo chini ausichiwambor@hotmail.com
Maoni yako Tima Kwa barua pepe au hapo chini ausichiwambor@hotmail.com
No comments:
Post a Comment