Monday, December 31, 2012

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI

TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI
Kila siku tunaimba mungu ibaliki Tanzania, watanzania wanaitikia“ ameeeeeeeeeeeeee”. Hii ndiyo Tanzania yetu. Mahakama inaonekana inapoteza kodi nyingi ksimamia kesi zisizo na kichwa wala miguu. Nasikitika kuona katiba ya Tanzania ya muungano ya 1977 Ibara ya 46-(1) inasema “Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshtaki au kuendesha mashtaka ya aina yeyote juu  yake mahakamani kwa ajili ya kosa la jinai”.
(2) “Wakati wote Rais atakapokuwepo madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhsiwa kufunga mahakama shauri kuhsu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama Raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku therathini kabla ya shauri kufungliwa mahakamani., Rais atapewa au atakuwa ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kfuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anuani yake ya mahari anopoishihuyo mdai na jambo hasa analodai”.
Katika ibara hii ya pili inampa Rais kinga kubwa dhidi ya madaraka ya Raisi. Kwa Tanzania inaonekana ukiwa Rais wan chi hii hwezi kushtakiwa na mahakama yeyote hata kama ukiboronga katika uongozi wako. Ukiamua kuua ni ruksa, kuwa mwizi ni ruksa, kufanya uhaini ni ruksa, uza madawa ya kulevya Ruksa, agiza watu Fulani wawekwe ndani Ruksa, kumpa kinga ya mtu kushtakiwa Ruksa? Jamani kweli tutafika kwa msingi huu. Kwa hali hii kwanini tusiseme kuwa Rais anaonekana kama yupo juu ya sheria na ndio ukweli halisi?
Kwa msingi huu watanzania kupata haki ya kumshtaki Rais itakuwa ndoto hadi tu pale katiba hii mpya inayotarajiwa kuandikwa 2014 na kupitishwa na wananchi itakapokamilika. Kwa sasa Rais katika awamu yake ya pili ya uchaguzi (Ungwe ya pili), wakati wa kampeni zake hata akitoa kauli za vitisho, Rushwa Takatifu, Kuiba kura na madudu mengine hawezi kushtakiwa hata kidogo? Jibu lipo katika ibara ya 46-(1 & 3).
(3), “isipokuwa kama akiacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A.-(1) itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa ameshika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba hii”.
Hapa ndipo ninaposema kuwa ukiwa Rais fanya chochote hata ukiondoka nani atakushtaki wakati una kinga “madhubuti” kutoka kwenye katiba yetu inayotuongoza ya mwaka 1977. kwa msingi huu hata mimi ijapokuwa sikuwa na ndoto ya kuingia kwenye siasa, unaweza kukuta nashawishika kuomba au Kutangaza nia miaka ya Mbele ili na mimi niwe Rais. Kwani nikiwa Rais nani atanishtaki? Kama wabunge kumi nawapendekeza mimi au kuwateua, chama changu kitakuwa na wabnge wengi wa kunitetea na hata nikifanya madudu nani ataniondoa?
Hata majaji wa mahakama kuu wenyewe nawateua mimi, mwanasheria mkuu namteua mimi na kumpa baraka yangu, Mkuu wa TAKUKURU namteua mimi, Kamishana wa Haki za binadamu na uongozi bora ni mimi. Hata wale wanaovaa zile nguo za kutisha wakuu wao nawateua mimi na kuwapendekeza vyeo mimi, mawaziri mimi, hata wale sisimizi nawateua mimi, hivi unadhani kuna mtu anaweza kunifungulia mashtaka wakati mimi nina kinga mzito kutoka kwenye katiba na wale niliowateua?
Hata kamishna wa haki za binadamu akipata taarifa zangu mbaya nilizofanya ataniambia Bwana Mkubwa hapa umebolonga mzazi. Lakini mimi ndio mwamuzi wa kusema nipelekwe mahakamani au nisipelekwe. Na kama waking’ang’ania watakuwa wanajihangaisha tu kwani hata leo hii nikimaliza uongozi wang nitaendelea kula bata (Msemo wa vijiweni yaani kula raha).
Na hata waqkipenda kunipeleka mahakamani Ibara ya 45 (1-a) Rais mpya hana haki ya kutoa msamaha juu ya shauri lolote lililopo mahakamani. Hivi kwa msingi huu kwanini nisitangaze nia na mimi. Lakini mimi si mwanasiasa na sina chama hata kimoja.
Hata ukiangalia namna ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais nayo ni utata mtupu. Kwa hiyo hapa simahanishi ukiwa Rais wan chi hii ufanye mambo kinyume na katiba, kwani ukitenda hayo kama Rais Bunge litakushtaki kama inavyoonyesha Ibara ya 46 (A). na ujue kwamba hata Waanchi wakichoka wanaweza kuandamana hata ikiwa kuna sheria ya kupinga maandano, watu waneweza kuandamana ili kuondokana na uozo wa uongozi.
Ni matumaini yangu kwamba mt yeyote atayechagliwa kuwa Rais, lazima aitetee na kuilinda katiba ya Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hata kama tunaitafuta nyingine ambao mimi napendekeza vifung nilivyoviandika kwenye nakala hii viondolewe ili kupunguza kinga ya Rais ya kutoshtakiwa.
“Watanzania wa leo sio wa jana. Na watanzania wa leo sio wa kesho”. Ninamaanisha kwa sasa upeo wa watu wa kufikiri ni mkubwa kuliko zamani. Hii ni kutokana na watu wa sasa wanasoma sana nakala mbalimbali kuliko zamani. Hivi itakuwa zaidi hapo baadaye kwani shule zetu za kata zitazalisha watoto wengi wenye uelewa mkubwa kuliko leo.
Sasa naamia upande wa Ubunge. Nakumbuka miezi kadfhaa iliyopita siku ya Wanasheria Tanzania duniani na Tanzania Rais wetu Dr. J. M. Kikwete alikili na kusisitiza kuwa baadhi ya taasisi muhimu zimokosa fedha kutokana na serikali kuishiwa fedha za kuendeshea taasisi hizo ili zitoe huduma vizuri kwa wananchi.
Moja ya Taasisi iliyoathirika sana kutokana na kauli yake ni hii ya mahakama. Lakini cha kushangaza ni kwamba fedha za kusimamia Ukiukwaji wa kampen za Ubunge fedha hizo zipo. Hakuna ida kabisa. Ni sanii mtupu. Hivi leo hii serikali inaweza kutoa fedha za kusimamia kesi ya uchaguzi nchi nzima, hii ni halali na fedha hizo ni kodi za wananchi.
Wananchi wanalipa kodi, wanapeleka idara ya Mahakama ili wawapaishe majina baadhi ya watu. Tusizungumze bila mifano angalia mfano huu “Mh. Tundu Lisu alipingwa ubunge mahakamani lakini alishinda, Mnyika Dar es Salaam pia Jana tarehe 24-05-2012 alishinda kama kawaida, na baadhi ya kesi nyingi zikiwemo zile za Mwanza na maeneo mengine.
Serikali kupitia mahakama wanamaliza fedha za bure. Napendekeza itungwe sheria kali itayowabana hawa wanaoshindwa kulipia fedia zote zilizotumika na mahakama katika kuendesha kesi ya aina hiyo. Kwa mtu anayeshindwa ndiye anayepaswa kulipa. Kwa kufanya hivi fedha za wanyonge na walipa kodi zitatumika kutoa hduma nyingine badala ya kendesha fedha za wachache wanaotaka kukuza majina kisiasa.
Kwa kawaida kesi moja ya ya kupinga matokeo inayopelekwa mahakama kuu ya Tanzania husimamiwa na majaji watatu waliobobea. Wanapokuwa huko hupewa posho mbalimbali ikiwemo maradhi, chakula na mengine. Hizi ni gharamu zisizotarajiwa. Hakuna ulazima wa kuzitumia hizi. Huu mimi naona ni ubadhilifu wa fedha za Umma.
   Napendekeza kwamba mahakama zisimamie kesi nyinginezo tofauti na hizi za sasa. Kwni kuna kesi nyingi zinasubiri majaji hawa watoe hukumu yake.
NAKALA HII IMEANDIKWA NA MSOMAJI WA GAZETI LA MWANAHALISI, CHIWAMBO AUSI R, TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU). ANASOMA BA-SOCIOLOGY AND SOCIAL WORK. 0753110740 NA E-MAIL ausichiwambor@hotmail.com

No comments:

Post a Comment