TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI
TANZANIA NA MAHAKAMA; KILIO CHA SAMAKI
Kila
siku tunaimba mungu ibaliki Tanzania,
watanzania wanaitikia“ ameeeeeeeeeeeeee”. Hii ndiyo Tanzania yetu. Mahakama inaonekana
inapoteza kodi nyingi ksimamia kesi zisizo na kichwa wala miguu. Nasikitika
kuona katiba ya Tanzania
ya muungano ya 1977 Ibara ya 46-(1) inasema “Wakati wote Rais atakapokuwa bado
ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshtaki
au kuendesha mashtaka ya aina yeyote juu
yake mahakamani kwa ajili ya kosa la jinai”.
(2) “Wakati wote
Rais atakapokuwepo madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhsiwa kufunga
mahakama shauri kuhsu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye
binafsi kama Raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila
tu kama angalau siku therathini kabla ya shauri kufungliwa mahakamani., Rais
atapewa au atakuwa ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kfuata
utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo
ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe,
jina lake na anuani yake ya mahari anopoishihuyo mdai na jambo hasa analodai”.
Katika ibara hii
ya pili inampa Rais kinga kubwa dhidi ya madaraka ya Raisi. Kwa Tanzania
inaonekana ukiwa Rais wan chi hii hwezi kushtakiwa na mahakama yeyote hata kama ukiboronga katika uongozi wako. Ukiamua kuua ni
ruksa, kuwa mwizi ni ruksa, kufanya uhaini ni ruksa, uza madawa ya kulevya
Ruksa, agiza watu Fulani wawekwe ndani Ruksa, kumpa kinga ya mtu kushtakiwa
Ruksa? Jamani kweli tutafika kwa msingi huu. Kwa hali hii kwanini tusiseme kuwa
Rais anaonekana kama yupo juu ya sheria na
ndio ukweli halisi?
Kwa msingi huu
watanzania kupata haki ya kumshtaki Rais itakuwa ndoto hadi tu pale katiba hii
mpya inayotarajiwa kuandikwa 2014 na kupitishwa na wananchi itakapokamilika.
Kwa sasa Rais katika awamu yake ya pili ya uchaguzi (Ungwe ya pili), wakati wa
kampeni zake hata akitoa kauli za vitisho, Rushwa Takatifu, Kuiba kura na
madudu mengine hawezi kushtakiwa hata kidogo? Jibu lipo katika ibara ya 46-(1
& 3).
(3), “isipokuwa kama akiacha kushika madaraka ya Rais kutokana na
masharti ya ibara ya 46A.-(1) itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua
mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa ameshika madaraka ya
Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba
hii”.
Hapa ndipo
ninaposema kuwa ukiwa Rais fanya chochote hata ukiondoka nani atakushtaki
wakati una kinga “madhubuti” kutoka kwenye katiba yetu inayotuongoza ya mwaka
1977. kwa msingi huu hata mimi ijapokuwa sikuwa na ndoto ya kuingia kwenye
siasa, unaweza kukuta nashawishika kuomba au Kutangaza nia miaka ya Mbele ili
na mimi niwe Rais. Kwani nikiwa Rais nani atanishtaki? Kama
wabunge kumi nawapendekeza mimi au kuwateua, chama changu kitakuwa na wabnge
wengi wa kunitetea na hata nikifanya madudu nani ataniondoa?
Hata majaji wa
mahakama kuu wenyewe nawateua mimi, mwanasheria mkuu namteua mimi na kumpa
baraka yangu, Mkuu wa TAKUKURU namteua mimi, Kamishana wa Haki za binadamu na
uongozi bora ni mimi. Hata wale wanaovaa zile nguo za kutisha wakuu wao
nawateua mimi na kuwapendekeza vyeo mimi, mawaziri mimi, hata wale sisimizi
nawateua mimi, hivi unadhani kuna mtu anaweza kunifungulia mashtaka wakati mimi
nina kinga mzito kutoka kwenye katiba na wale niliowateua?
Hata kamishna wa
haki za binadamu akipata taarifa zangu mbaya nilizofanya ataniambia Bwana
Mkubwa hapa umebolonga mzazi. Lakini mimi ndio mwamuzi wa kusema nipelekwe
mahakamani au nisipelekwe. Na kama
waking’ang’ania watakuwa wanajihangaisha tu kwani hata leo hii nikimaliza
uongozi wang nitaendelea kula bata (Msemo wa vijiweni yaani kula raha).
Na hata
waqkipenda kunipeleka mahakamani Ibara ya 45 (1-a) Rais mpya hana haki ya kutoa
msamaha juu ya shauri lolote lililopo mahakamani. Hivi kwa msingi huu kwanini
nisitangaze nia na mimi. Lakini mimi si mwanasiasa na sina chama hata kimoja.
Hata ukiangalia
namna ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais nayo ni utata mtupu. Kwa hiyo
hapa simahanishi ukiwa Rais wan chi hii ufanye mambo kinyume na katiba, kwani
ukitenda hayo kama Rais Bunge litakushtaki kama
inavyoonyesha Ibara ya 46 (A). na ujue kwamba hata Waanchi wakichoka wanaweza
kuandamana hata ikiwa kuna sheria ya kupinga maandano, watu waneweza kuandamana
ili kuondokana na uozo wa uongozi.
Ni matumaini
yangu kwamba mt yeyote atayechagliwa kuwa Rais, lazima aitetee na kuilinda
katiba ya Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania
ya mwaka 1977 hata kama tunaitafuta nyingine
ambao mimi napendekeza vifung nilivyoviandika kwenye nakala hii viondolewe ili
kupunguza kinga ya Rais ya kutoshtakiwa.
“Watanzania wa
leo sio wa jana. Na watanzania wa leo sio wa kesho”. Ninamaanisha kwa sasa upeo
wa watu wa kufikiri ni mkubwa kuliko zamani. Hii ni kutokana na watu wa sasa
wanasoma sana
nakala mbalimbali kuliko zamani. Hivi itakuwa zaidi hapo baadaye kwani shule
zetu za kata zitazalisha watoto wengi wenye uelewa mkubwa kuliko leo.
Sasa naamia
upande wa Ubunge. Nakumbuka miezi kadfhaa iliyopita siku ya Wanasheria Tanzania
duniani na Tanzania Rais wetu Dr. J. M. Kikwete alikili na kusisitiza kuwa
baadhi ya taasisi muhimu zimokosa fedha kutokana na serikali kuishiwa fedha za
kuendeshea taasisi hizo ili zitoe huduma vizuri kwa wananchi.
Moja ya Taasisi
iliyoathirika sana
kutokana na kauli yake ni hii ya mahakama. Lakini cha kushangaza ni kwamba
fedha za kusimamia Ukiukwaji wa kampen za Ubunge fedha hizo zipo. Hakuna ida
kabisa. Ni sanii mtupu. Hivi leo hii serikali inaweza kutoa fedha za kusimamia
kesi ya uchaguzi nchi nzima, hii ni halali na fedha hizo ni kodi za wananchi.
Wananchi
wanalipa kodi, wanapeleka idara ya Mahakama ili wawapaishe majina baadhi ya
watu. Tusizungumze bila mifano angalia mfano huu “Mh. Tundu Lisu alipingwa
ubunge mahakamani lakini alishinda, Mnyika Dar es Salaam
pia Jana tarehe 24-05-2012 alishinda kama
kawaida, na baadhi ya kesi nyingi zikiwemo zile za Mwanza na maeneo mengine.
Serikali kupitia
mahakama wanamaliza fedha za bure. Napendekeza itungwe sheria kali itayowabana
hawa wanaoshindwa kulipia fedia zote zilizotumika na mahakama katika kuendesha
kesi ya aina hiyo. Kwa mtu anayeshindwa ndiye anayepaswa kulipa. Kwa kufanya
hivi fedha za wanyonge na walipa kodi zitatumika kutoa hduma nyingine badala ya
kendesha fedha za wachache wanaotaka kukuza majina kisiasa.
Kwa kawaida kesi
moja ya ya kupinga matokeo inayopelekwa mahakama kuu ya Tanzania husimamiwa na majaji
watatu waliobobea. Wanapokuwa huko hupewa posho mbalimbali ikiwemo maradhi,
chakula na mengine. Hizi ni gharamu zisizotarajiwa. Hakuna ulazima wa kuzitumia
hizi. Huu mimi naona ni ubadhilifu wa fedha za Umma.
Napendekeza
kwamba mahakama zisimamie kesi nyinginezo tofauti na hizi za sasa. Kwni kuna
kesi nyingi zinasubiri majaji hawa watoe hukumu yake.
NAKALA HII
IMEANDIKWA NA MSOMAJI WA GAZETI LA MWANAHALISI, CHIWAMBO AUSI R, TEOFILO KISANJI UNIVERSITY
(TEKU). ANASOMA BA-SOCIOLOGY AND SOCIAL WORK. 0753110740 NA E-MAIL ausichiwambor@hotmail.com